Uwezeshaji Lugha ili Kuleta Maendeleo: Sera, Utendaji na Nafasi ya Kiswahiili

Citation:
Michira N, IRIBEMWANGI PI, Mbatia M, Mutiga J. "Uwezeshaji Lugha ili Kuleta Maendeleo: Sera, Utendaji na Nafasi ya Kiswahiili.". In: Ukuzaji wa Kiswahili. Nairobi: Focus Publishers Limited; 2014.

Abstract:

Uwezeshaji Lugha ili Kuleta Maendeleo: Sera, Utendaji na Nafasi ya Kiswahili
Jayne Mutiga
Ikisiri
Nafasi ya lugha za waliokuwa wakoloni Afrika kama vile; Kiingereza, Kifaransa na Kireno, imezisukuma lugha za Kiafrika hadi ukingoni katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi barani Afrika. Lugha za Kiafrika zimevurugwa na kutengwa katika msitari wa mbele wa uchumi wa nchi ambapo lugha hizi zinazungumzwa, jambo ambalo linaonekana kuwa mojawapo ya visababishi vya Afrika kutokuwa na maendeleo. Jambo hili limesasababishwa na nafasi ya lugha zilizokuwa zinatumiwa na wakoloni, kama vile Kiingereza, Kifaransa na Kireno na kuendelezwa na mtazamo wa waafrika wenyewe ambao huzidunisha lugha zao na kuamini kwamba wataweza kujiendeleza kupitia kumilisi vyema na kutumia lugha zilizotumiwa na serikali za kikoloni; jambo hili pamoja na wazo kuwa lugha ndiyo msingi au nguzo ya mchakato wa maendeleo ya namna yoyote ile. Swali la kujiuliza ni: Je, bara la Afrika linaweza kujipatia maendeleo yaliyo thabiti wakati wazungumzaji wanaendelea kutumia lugha ambazo zinaonekana kuzuia kuelimishwa pamoja na mawasiliano miongoni mwa watu wengi? Hivyo basi, lengo la makala haya ni kuangazia vile lugha inaweza kuwezeshwa ili kusaidia watumizi wake kushiriki katika shughuli za maendeleo ya nchi yao. Aidha inaendelea kuangazia njia ambazo zinaweza kutumiwa kuwezesha lugha ya Kiswahili nchini Kenya na katika eneo la Afrika Mashariki ili kuendeleza eneo hili wakati huu ambapo kuna katiba mpya na uundaji sera mpya nchini Kenya.

UoN Websites Search